hatua za uombaji wa E-Passport

Kabla ya kujaza Fomu Mwombaji ahakikishe anaskani picha yake (passport size) na viambatanisho vyote (Cheti cha kuzaliwa, nakala ya pasipoti, cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo (affidavit] ya Baba au Mama mzazi wa mwombaji mwenye uraia wa Tanzania na kitambulisho cha uraia kama anacho). Viambatanisho hivyo viwe kwenye mfumo wa picha (image. jpeg, jing) na kila kiambatishi kisizidi ukubwa wa 1 MB. Viambatanisho hivyo atatakiwa kuvipakia (upload) wakati anajaza fomu.

Awe na kadi yake ya benki ambayo atatumia kufanya malipo wakati wa kujaza fomu hiyo.

Mwombaji ajaze fomu katika mtandao (online) kupitia kwenye tovuti ya Idara ya Uhamiaji utaona sehemu ya kupata fomu ya maombi ya pasipoti (passport application form).

Baada ya kujaza mwombaji atatakiwa kulipa Ada ya dola Tisini (90) kupitia Ankara (bill) atakayopewa ambayo itakuwa na namba ya udhibiti (control number).

Ankara hiyo ya malipo itamwonyesha “link” ya kufanya malipo kwa njia ya mtandao https://epay.gepg.go.tz

Kwenye “link” hiyo ataweka namba ya udhibiti (control number) na kiasi cha malipo kama Ankara (bill) inavyoonesha.

Akikamilisha kujaza fomu na malipo mwombaji anashauriwa kutuma nakala ya fomu ya maombi, risiti ya malipona viambatisho husika ili vihakikiwe na kupangiwa miadi ya kuja Ubalozi kwa ajili ya kupiga picha pamoja na kuchukuliwa alama za vidole. Tumia barua pepe ifuatayo: consular@tzembassy.kr

Pasipoti ikipokelewa kutoka Uhamiaji, Dar es Salaam/ Zanzibar, mhusika atatakiwa kuifuata mwenyewe Ubalozini, Seoul.

UBALOZI WA TANZANIA, SEOUL

tanzania embassy, seoul

Address: 4th floor, Vivien Corp. Building 52,Seobinggo-ro 51 gil, Yongsan-gu,
Tel: (+82-2) 793 - 7007, Fax Number : (+82-2) 795 - 8990, E-mail Address: info@tanzaniaembassy.kr

Webmaster & Developer: Gowelle John

Copyright © 2021 Tanzania Embassy, Seoul