Post Preview Image

Seoul Africa Festival

Summary:

2019/5/25 tulikuwa na Maonyesho ya Seoul Africa Festival yanayoandaliwa na NGO ya Africa Insight. Maonyesho hayo kwa mwaka huu yameshirikisha nchi zote za Africa, Korea Africa Foundation, Cultural Associations na Makampuni yanayofanya kazi na Nchi za Africa.

 

Nchi za Kiafrika ziliwakilishwa kwa Hotuba kutoka kwa Dean wa African Ambassadors Bal. Carlos Boungou, Balozi wa Gabon.

 

 

Mhe. Balozi alishiriki katika Ufunguzi, na baadae kujiunga na Watanzania ktk maonyesho hayo.

 

 

 

Tanzania kama kawaida imeshiriki vyema kwa kuwa na mabanda mawili, la Ubalozi na lile la Diaspora. Tumeweza kutangaza Utalii na pia Utamaduni wa Mtanzania, na kulikuwepo na food stalls za Kuuza vyakula vya Kitanzania. Pilau, Maandazi, kuku choma, Chips mayai, Kahawa, Juice ya Alovera, nk vilikuwepo. Pia kilikuwa na Tingatinga, Vinyago, kahawa, na mambo ya Ususi. Tanzania iliwakilishwa vyema.

tanzania embassy, seoul

Address: 4th floor, Vivien Corp. Building 52,Seobinggo-ro 51 gil, Yongsan-gu,
Tel: (+82-2) 793 - 7007, Fax Number : (+82-2) 795 - 8990, E-mail Address: info@tanzaniaembassy.kr

Webmaster & Developer: Gowelle John

Copyright © 2021 Tanzania Embassy, Seoul